Friday, 26 May 2017

UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI


Ufugaji huu ni wa kienyeji kabisa ila huu umeboreshwa kidogo ili kuleta faida zaidi, kwanza itabidi uwe na eneo lakutosha,banda la kuku liwe linalohamishika au liwe limejengwa juu juu, hii husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa kwa sababu kinyesi cha kuku kikilundikana huweza kubeba vimelea vya magonjwa au liwe banda kubwa ambalo lina ngazi au mapumba chini ya sakafu ya banda kuepuha magonjwa.

AINA YA UFUGAJI WA KUKU.
1.Kufugia Huria.
Kuku huachwa wenyewe kujitafutia chakula na maji.Njia hii inatumika zaidi kufugia kuku wa kienyeji.Mara chache sana mfugaji huwapatia chakula cha ziada.
Ufugaji huu lazima uwe na eneo la kutosha kuku kuzunguka na kutafuta chakula.
Faida zake
Ø Ni njia rahisi ya kufuga.
Ø Gharama yake pia ndogo
Ø Kuku wanapata mazoezi ya kutosha.
Ø Kuku wanapata chakula mchanganyiko abacho kinafaa kiafya.
Hasara zake
Ø Kuku wanakuwa hatarini kuibiwa au kudhurika na wanyama wakali na hali mbaya ya hewa.
Ø Ukuaji wa kuku ni hafifu hufika uzito kilo 1.2 baada ya mwaka.
Ø Nirahisi kuambukizwa magonjwa.
2.Kufuga nusu ndani-nusu nje (Semi-intensive)
Huu ni ufugaji ambao kuku wanakuwa na bandalililounganishwa na uzio kwa upande wa mbele.
Hapa kuku wanaweza kushinda ndani ya banda au nje ya banda wakiwa ndani ya uzio.
Faida zake
Ø Kuku wanakuwa salama mbali na madui mbalimbali
Ø Utaweza kuwalisha kuku vizuri hivyo wataweza kuongeza uzalishaji wa mayai na nyama ( kwa kukua haraka )
Ø Itakuwa rahisi kwako kudhibiti wadudu na vimelea vinavyoweza kuleta magonjwa kwa kuku.
Ø Ni rahisi kuwatenganisha kuku kwa makundi tofautitofauti na kuwaudumia ipasavyo.
Ø Rahisi kuwatambua kuku wagonjwa kuliko kufugia huria.
Changamoto za kufugia nusu ndani nusu nje.
Ø Hauna budi uwe na mda wa kutosha kwa ajili ya kuwahudumia kuku wako.
Ø Pia utaitaji kuwa na eneo kubwa kiasi cha kutosha kufugia
Ø Pia utahitaji kuingia Gharama ya ziada kidogo ya kutengeneza wigo na banda na kuwapatia kuku chakula cha ziada .
Ø Utahitaji kuwa na vifaa vya kulia chakula na maji

3. Kufugia ndani ya Banda tu.
Njia hii kuku huwa ndani ya banda tu, Katika njia hii kuku hukaa ndani ya banda mda wote,
Njia hii ya ufugaji utumiwa na wafugaji wa kuku wa kiasasa kama (Broiler for meat purpose and Layer for egg production)  
Lakini unaweza kutumika hata kuku wa asili hasa sehemu zenye ufinyu wa maeneo.
Faida zake
Ø Nirahisi kutambua na kudhibiti magonjwa.
Ø Ni rahisi kudhibiti upotevu wa kuku,mayai na vifaranga
Ø Ni rahisi kuwapatia chakula kulinga na mahitaji ya kila kundi.
Ø Ni rahisi kuwatambua na kuwaondoa kuku wasiozalisha Katika makundi.
Changamoto za Ufugaji wa Ndani ya Banda tu.
Ø Unatakiwa uwe na mda wa kutosha wa kuwahudumia kuku wako kikamilifu.
Ø Pia unatakiwa kuwa na mtaji mkubwa wa kujenga banda na kuwanunulia kuku chakula.
Ø Ugonjwa ukiingia ni rahisi kuambukizana. Vilevile kuku huweza kuanza tabia ya kudonoana.
NB; Ni muhimu kuhakikisha kuku wako wanapata chakula cha kutosha chenye virutubisho vyote vinavyohitajika unapoamua kutumia mfumo wa ufugaji wa kuku wa ndani.
 
BANDA BORA
Banda liwekewe viota vya kutagia na unaweza kuwafundisha kuku kuvitumia mapema kabla ya kuanza kutaga kwa kuchelewa kuwafungulia asubuhi. Kwa kawaida kuku hupenda kulala bandani wakiwa juu juu kwa hiyo uweke baadhi ya fito au mbao nyembamba zikining’inia pia kuwe na vyombo vya chakula nje ya banda
Hakikisha banda halivuji na wanyama wakali hawaingii lakini liwe na hewa ya kutosha na lisiwe na joto wala baridi kali, ni vizuri ukiliweka chini ya miti
Ili kuboresha ufugaji huu inashauriwa kutumia majogoo ya kisasa ambayo yana patika kwa mazalishaji wa kuku kote nchini, pia unaweza kutumia majogoo ya kuku aina ya
KUCHI wanaopatikana zaidi miko ya Singida na Shinyanga. Majogoo ya kisasa huweza kuhudumia wastani wa majike 20-25 na KUCHI huweza kuhudumia majike 10 -15 kwa sababu ni wavivu kidogo
Andaa na banda la kukuzia watoto ambalo litawakinga na wanyama wakali na mwewe, banda linakuwa wazi juu hukulikizuiwa na waya kwa 75% na 25% iwe imezibwa kwa mbao ili kuwapatia kivuli wanapohitaji, banda hili lina hitaji kuhamishwa hamisha angalau mara 5 kwa siku kutika mahali pamoja hadi pengine, hakikisha banda la watoto lina maji na chakula muda wote, pia kumbuka kuwawekea mabaki ya mboga za majani kama mchicha, kunde, kisamvu n.k

Banda hili pia waweza tumia kwa kukuzia vifaranga au kutagia mayai.


Banda hili linaanza kujenjwa kwa matofali kwenye msingi.
Mahitaji ya kujenga banda hii
Ø Mabati
Ø Misumali
Ø Mbao
Ø Tofari
Ø Sumenti
Ø Wirenet au waya wa Senyenje na hii itasababisha kuku kupata hewa ya kutosha

MABANDA YA KISASA
Banda hii linauzo wa kufuga kukuhadi 3000
























Upana 10 m*Urefu 80m
Mahitaji yakujenga Banda hii
Ø Eneo 1300m kwa (semi-intensive)
Ø Mabati
Ø Mbao
Ø Senyenge wire
Ø Tofali kwaajili ya msingi
Ø Sumenti
Ø Misumali
Banda lenye uwezo wa kuku 600

Upana 5m*urefu 20m
Mahitaji ya Banda hii
Ø Eneo 150m
Ø Mabati
Ø Wire
Ø Mbao
Ø Matofali
Ø Sumenti
Ø Misumali
  • CHANJO ZA KUKU
Kuku wapewe chanjo ya kideri/mdondo kila baada ya miezi mitatu chanjo hii hupatikana nchini kote ukifika dukani ulizia chanjo ya newcastle, utapata maelekezo ya jinsi ya kuwawekea kuku kwenye maji ya kunywa, chanjo hii wapewe kuku wazima tu na wagonjwa watengwe mbali
  • MINYOO YA KUKU 
Kuku hunyweshwa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, kuna dawa kama piperazine na nyinginezo ambazo huwekwa kwenye maji
  • CHAWA NA UTITIRI
Unaweza kutumia dawa za kuogeshea mifugo kama ecotix au dawa ya unga unga ya kunyunyuzia kama akheri powder, dawa ya akheri unaweza kuimwaga bandani na kisha kumnyunyuzia kuku mwilini ukiwa umemning’iniza kichwa chini miguu juu ili mayoya yaacha nafasi ya dawa kuingia
  • MAGONJWA YA MAPAFU
Kuna magonjwa mengi yanayoshambulia mfumo wa hewa, dawa ya tylosin inauwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa karibu yote, wape dawa hii mara tu unapoanza kuona dalili za mafua
MAGONJWA YA KUKU,DALILI, NA TIBA ZAKE
Kila ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha na magomjwa mengine, ingawa zipo zile za kufanana mfano kutokula vizuri, kushusha mabawa, kuzubaa/kusinzia na joto kuwa juu
 NEWCASTLE /KIDERI / MDONDO
Dalili kuu: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba. kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30% na mult vitamini.
GUMBORO / INFECTIOUS BURSAL DISEASE.
Dalili kuu:Kuharisha rangi nyeupe kama chokaa. Ukimpasua baada ya kufa kunakuwa na kama matone ya damu kifuani na kwenye firigisi sehemu ya mbele
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.
MAREK'S DESEASE/ MAHEPE
Dalili kuu:kuparalyse /kukakamaa and kwa miguu na mabawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kihifadhia chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5 wakianza kutaga.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.
NDUI YA KUKU / FOWL POX.
Dalili kuu:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya kama vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba., kupunguza madhara waoshe kwa maji ya uvugu vugu yenye chumvi ya mawe hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic kama Otc 20%.
 MAFUA MAKALI/ INFECTIOUS CORYZA
Dalili kuu:Chafya, kusinzia, kuvimba sehemu za  uso, kichwa  na macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, udenda puani na mdomoni.
Tiba: Fluban, au  Tylodox au OTC 20 %, Tylosan, changanya na mult vitamini.
 FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO
Dalili Kuu:Mharo rangi ya njano.
Tiba: Esb3, Trimazine 30%, Tylodox.

COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU.
Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu.
Tiba: Amprolium 20%,Esb3, Trimazine 30%, Vitacox, na Agracox.
FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU.
Dalili kuu: kinyesi mharo wa kijani.
Tiba: Trimazine 30 % au Esb3.
MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKANAYO NA LISHE DUNI
Dalili kuu:Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.
Tiba: Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa mult vitamin na protein, kwa wanaodonoana kata au choma midomo yao na uwape mboga za majani ukiwa umezining'iniza juu kidogo.

VYAKULA
Vifaranga
Vifaranga
Kuku
Anza
Kuzia
Mayai taga
Kiasi(kg)
kg
kg
kg
Mahindi sagwa
38
28
20
Pumba mahindi
19
24
30
Pumba mpunga
19
24
30
Mashudu alzeti
08
08
06
Mashudi Pamba
00
02
06
Dagaa sagwa
10
07
03
Damu sagwa
04
05
02
Chokaa Mifugo
01
01
02
Madini Mchanganyiko
0.5
0.5
0.5
Chumvi sagwa
0.5
0.5
0.5
Jumla
100kg
100kg
100 kg
NB:
Kama utawapa kuku wako wa wanaotaga mayai dawa zenye sulphur ndani watapunguza kutaga mayai, kwa hiyo kama utaweza kupata dawa ambayo haina sulphur ndani yake itakuwa ni vizuri zaidi.


agriculturecomlizy.blogspot.com
agriculturecomlizy.blogspot.com
Prepared, 
KILIMO BORA,
Agriculture Field Officer
Faraja Israel Lwoga.
phone: +2557198886932.





No comments:

Post a Comment

AGRICOMLIZY®

KILIMO CHA MAHINDI

MAHINDI Mahindi ni zao muhimu sana katika kilimo hapa nchini na hukuzwa na takribani 70 % ya wakulima wa hapa Tanzania. Maeneo yanayoongo...