1.
UZARISHAJI BORA WA MITIKI
http://agricomlizy.blogspot.com
By
Faraja Israel Lwoga
Mitiki ni mti unaotengemewa na watu wengi kutokana na ubora wake
hasa katika uimara wa mbao zake kwani huteleza na hung’aa sana pia mchwa
hawawezi kushambulia mti huu, Jina kamili ni (Teak tree)
tectonagrandis.
UANDAJI WA MBEGU
UANDAJI WA MBEGU
Ø Mbegu ya mtiki
inatakiwa kulowekwa kwenye maji kwa siku tatu na kila baada ya masaa kumi na
mbili unamwaga maji na kuweka mengine hii ni kwasababu ya kuondoa sumu iliyo
kwenye maganda yake ya nje kwa sababu ni magumu ambayo mche hauwezi kutoka
kiurahisi, Au unaweza kusugua maganda kwa kutoa (hard cort) ngozi ngumu ya
mbegu ya mtiki baada ya kufanya hivyo unawaga kwenye kitaru kilicho tayarishwa
vizuri kulingana na idadi ya miche unayohitaji kuotesha unaweka (farm yard
manure) mbolea ya ngombe au ya kuku, au udongo wenye lutuba ambao ni mweusi (dark
soil).
Njinsi ya kuaandaa
udogo wa kuchanganya ni udogo wa
msituni,mbole za wanyama kama kuku,ng’ombe,mbuzi n.k ,pumba za mpunga na
mchanda (forest
soil,manure,rice polish&sand) kwa uwiano wa 3:2:1:1 hii itasadia mmea kupata
hewa ya kutosha kwenye viriba na kuhifadhi unyevu vizuri kwenye viriba yako
mkulima,
- Unamwagilia maji kabla ya kusia mche au mbegu, unaweza kupanda moja kwa moja mbegu au kupanda miche kutoka kwenye kitaru chako kilicho tayarishwa vizuri.
UPANDAJI WA MTIKI
Upandaji wa mitiki huafanyika mara baada ya mvua za kwanza
kuanza kwa sababu ukuaji wa miche midogo huitaji mvua za kuendelea kwa kipindi
kirefu, pia mvua za kwanza huwa na nitrogen ya kutosha kusaidia ukuaji
wa mimea.
- Vipimo vya upandaji kati ya mche na mche ni mita 2.5 mpaka 3, kama utatumia kipimo cha mita 3 kwa 3 ekari moja (mita 70 kwa 70) itaingia miche 530 kwa wastani. Miche ya mitiki hubananishwa wakati wa upandaji ili kuisaidia ikue kwa kunyooka kwenda juu ingawa mingine ya katikati itapunguzwa baada ya miaka 5-6 kuipa nafasi ile iliyobaki kama 260 iweze kunenepa zaidi.
- Mashimo ya mitiki hayahitaji kuchimbwa kabla kwa sababu yanaweza kufukiwa na mvua, kwa kawaida mashimo haya yana kuwa na urefu usiozidi futi moja (urefu wa rula ya mwanafunzi yaani cm 30) kwa hiyo siku ya upandaji wachimbaji wa mashimo ndio wawe wapimaji wa nafasi kati ya mti na mti. Wale wapandaji wahakikishe kwamba sehemu ya mzizi inakuwa chini ya ardhi na imefunikwa na udongo yote na sehemu ya shina inakuwa juu.
- Miti kishapandwa iachiwe sehemu kidogo ya kisahani kwa ajili ya kuhifadhia maji kidogo, nyasi kidogo zinaweza kuwekwa kuzunguka shina ili kuzuia unyevu kunyonywa na jua (evaporation) ingawa hii wakati mwingine inaweza kuwavutia mchwa wakashambulia miche yako.
- Miche ikianza kuchipua baada ya siku chache vichipukizi zaidi ya kimoja vitachipua, hapa inatakiwa uvikate vyote na kubakiza chenya afya (viwili vitakuwa sawa)
Upandaji wa mitiki
hufanyika katika namna mbili, wa kwanza ni ule wa kupanda miche ikiwa mizima
kutoka katika vifuko na ya pili ni kutumia miche toka
kwenye kitalu ambako inashauriwa kuing'oa na kisha kukata
sehemu ya mzizi na shina, ambako utabakiwa na mzizi 70% na
shina 30%.
Kitaalamu miche iliyokatwa na kubaki kama vipandikizi ina sifa mbili kubwa
Miche ikiwa kwenye vifuko safi kwaajili ya kukua |
(a) Miche itakayoota katika vipandikizi hivi ina uwezo mkubwa wa
kuhimili ukame iwapo kutakuwa na upungufu wa mvua za msimu wakati wa upandaji.
Mara nyingi miche ikipandwa kwenye mvua pungufu hufa sehemu ya juu ya
shina/mche na sehemu ya chini ya mzizi kama vile miti inavyopukutisha majani,
na hii husaidia kuhifadhi maji ndani ya mmea. Sasa kabla hili halijatokea sisi
tunakata kabisa hizo sehemu zitakazo kufa iwapo kutakuwa na mvua pungufu.
(b) Miti inayoota katika vipandikizi inaasilimia kubwa zaidi ya
kukua kwa kunyooka kwenda juu, wakati miti iliyokulia kwenye vifuko ina uwezo
zaidi ya kupinda kwa sababu wakati wa uotaji ikiwa midogo, miche hushindana
kukua na kukimbilia mwanga wa jua. Wakati huu ndio mche huanza kupinda kufuata
mwanga ili kushindana na ile iliyokua haraka. Ili kuepuka hili, kata miche yako
na ianze kuchipua upya ikiwa shambani kwenye nafasi.
Vipandikizi vilivyokatwa vinauwezo wa kukaa mpaka siku 7 bila
kufa hadi siku ya kupandwa shambani, kwa maana hiyo unaweza kuvisafirisha toka
mkoa mmoja hadi mkoa mwingine kwenda kuvipanda. Kama utakuwa umeandaa
vipandikizi vyako na mvua zikawa bado kuanza, weka udongo kwenye chombo
chochote mwagia maji kidogo (yasituame) halafu
chomeka vipandikizi vyako na usubiri siku ya mvua kuanza ili ukavipande
Kabla ya kupanda
miche ya mitiki shamba ni lazima liwe limeandaliwa, uandaaji wa shamba ni
lazima ufanyike mapema kabla ya mvua kuanza kunyesha kwa sababu upandaju huanza
mara baada ya mvua za kwanza kunyesha.
Uandaaji wa shmba la mitiki ni wakawaida kama ule wa mashamba mengine, visiki
vyote ni lazima ving'olewe kisha majani yote yalimwe na ikiwezekana yatiwe moto
kwa umakini wa hali ya juu kuepusha madhara ya moto.
Kama ulimaji utakuwa ni wa trekta au kutumia jembe la kukokotwa na wanyama
(plau) hii ni nzuri zadi kwa sababu majani yatafukiwa ardhini na kuongeza
rutuba kwenye udongo. Uuaji wa magugu kwa kutumia madawa kama Round up wanamazingira
huwa hatushauri, ingwa ni njia moja ya haraka na nafuu zaidi kuliko kulima kwa
jembe lolote lile.
Kwa ukanda wa pwani mvua za masika huanza kati ya mwezi wa 3 - 4 kwa hiyo ni vizuri sana kama utaanza kuandaa shamba kwenye
mwezi wa 2 (February) na
mvua za vuli huanza kwenye mwezi wa 11 (November) kwa
hiyo shamba liwe tayari kwenye mwezi wa
10 (October)....
Mkurugenzi |
Kwa msaada zaidi
Wasiliana nami kupitia
+255719 886 932
Email: flwoga_9196@outlook.com
flwoga629@gmail.com
flwoga629@gmail.com
No comments:
Post a Comment