Friday, 27 September 2019

KILIMO CHA MAHINDI

MAHINDI
Mahindi ni zao muhimu sana katika kilimo hapa nchini na hukuzwa na takribani 70 % ya wakulima wa hapa Tanzania.
Maeneo yanayoongoza kwa kulima mahindi ni nyanda za juu kusini kama Songea,Sumbawanga,Mbeya,Njombe,Iringa n.k. Ni chakula cha kila siku cha watanzania wengi hukuzaji wake  hutegemea matukio mbali mbali yakijumuisha kunyesha kwa mvua sana sana pia bei, upatikanaji wa pembejeo za kilimo mfano:- Mbolea,Sumu ya mmea,viua dudu.
Kunahaja ya kuboresha  ukulima wa mahindi ikizingatiwa kuhitajika sana kwa nafaka hii muhimu nchini na hata nje ya Tanzania kama haikikisho la kuweko kwa chakula cha kutosha. Kwa mahitaji haya lazima kuweko njia madhubuti  haza mbegu bora,dawa za palizi za magugu,viua dudu na elimu shilikishi kwa watalamu wa kilimo (Maafisa Kilimo) kwakupata mafunzo ya mbegu bora na viwatilifu bora ambavyo vitamsadia mkulima kulima kilimo chenye tija.

 UTHIBITI WA MAGUGU
Kwa wakulima wengi wanatanzania wanatumia jembe la mkono kufanya palizi hii ni njia nzuri lakini haiokoi mda zaidi na kuupa mmea wa muhindi ufanisi mzuri wa kubeba mahindi vizuri haza magugu yakichanganyana na mahindi, lakini wanaweza kutumia dawa kuthibiti magugu hasa kabla mahindi yajatoka,
Wakulima wanaweza kutumia Dual Dold wakiwa wanachanganya na maharagwe pamoja yaani kilimo mchanganyiko au wanaweza kutumia dawa ya magugu ya Primagram Gold  kwajili ya palizi kwenye mahindi kutoka kampuni ya syngenta ( www.syngenta.com) ambayo hutumika kwa mahindi bila kuchanganya na maharagwe unatumia mls 300 kwa lita 20 za maji na unapulizia ikiwa umeshapanda mbegu chini na udongo kuwa na unyevunyevu wa kutosha kushikana na dawa vizuri.

www.agricomlizy.blogspot.com
Picha hiyo juu inaonesha shamba la mahindi ambalo limetumia Primagram Gold na mbegu ya mahindi ya Sy 644 ukanda wa juu kusini # Iringa Tanzania. Dawa hii ambayo halijawahi kuingizwa jembe ndani ya miezi miwili na wiki tatu dawa hii huwafaa wakulima wanaolima mwaka nenda mwaka rudi kwa ufanisi wa hali ya juu zaidi kuliko dawa zingine zozote.




















Picha ambazo zinaonesha usadikisho wa Primagram Gold jinsi inavyofanya kazi vizuri na kuleta mazao yenye afya nizuri.

UTHIBITI WA VIPEKECHA BUA
( Viwavi jeshi,Viwavi jeshi vamizi, Panzi n.k)
Kuna dawa mbalimbali ambazo zinawaangamiza vizuri wa viwavi vamizi na wadudu wa halibifu wa hasa mahindi yakiwa madogo apa tumia dawa kama Karate,Match,Dkluf,Profecron n.k ila dawa ya Viwavijeshi vamizi(luhoma) tumia Match kutoka syngeta www.syngenta.com  dawa hii inauwa yai lava na kipepeo pia yaani inaufanisi wa hali  ya juu uchanganyaji ni mls 25 kwa lita 20 za maji.

Picha hii inaonesha utambuzi wa mdudu viwavijeshi vamizi kanda za juu kusini na Agronomist Lwoga kwaajili ya kutafuta dawa stahiki ya kupiga hasa kumthibiti viwavijeshi vamizi.


MBEGU CHOTARA ZA MAHINDI.
Mbegu za mahindi bora zipo nyingi sana, neno chotara ni mbegu za kisasa zilizo ongezewa ufanisi wa utoaji mavuno mengi sana na kustahimili hali ya hewa mbalimbali hapa ni uchaguzi wa eneo la kupanda hizo mbegu yaani ukanda wa mvua nyingi au chache ambazo zitakuwezesha uchaguzi wa mbegu ipi upande kuna mbeguz amda mfupi na mda wa kati na mda mrefu.
Za mda mfupi ni Sy 514 kutoka syngenta,Tumbili,Pundamilia, za mda wa kati ni Sy 634,Simba n.k za mda mrefu ni Sy 644,Tembo,DK 777 n.k.
na upandaji ni 25cm mhindi kwa muhindi na mstari 80 cm au 30cm kwa 75 hii ni nafasi nzuri sana kwa punje mojamoja.
Picha hiyo ikionesha nafasi nzuri kati ya mhindi na mhindi na pia mstari na mstari ,

MMEA UNAHITAJI NINI KUISHI?

      VIRUTUBISHO VYA MIMEA


Virutubisho vya mimea vimegawanyika katika makundi matatu

1. VIRUTUBISHO MSINGI

Hivi ni virutubisho vinavyohitajika kwa kiwango kikubwa na kila mmea ili uweze kuzaa mazao yenye tija.

2. VIRUTUBISHO SEKONDARI

Hivi ni virutubisho ambavyo vinahutajika kwa kiasi kikubwa na baadhi tu ya mimea.

3. VIRUTUBISHO VIDOGOVIDOGO

Hivi ni virutubisho vinavyohitajika na kila mimea kwa kiwango kidogo ila vikikosekana vinaweza kuleta madhara kweny ukuaji wa  mimea



v  VIRUTUBISHO MSINGI

1.NITROGEN (N)

Hiki ni kirutubisho muhimu sana  husaidia  mimea yafuatayo:

·         kukuza mmea

·         kuupa mmea rangi ya kijani 

UPUNGUFU: mmea kuwa wa njano hasa majani makubwa

KUZIDI: Mmea hurefuka sana na  kuwa dhaifu

UPATIKANAJI:  Mbolea ya DAP,NPK,CAN.UREA

Upungufu wa Nitrogeni kwenye Mahindi.






2. PHOSPHOROUS (P)

Kirutubisho hiki  husaidia mmea yafuatayo:-

·         Kutengeneza mizizi,

·         husaidia  utengenezaji wa  punje na ukuaji wa tunda



UPUNGUFU: Mmea kuwa na rangi ya zambarau

KUZIDI:  huathiri  upatikanaji wa virutubisho vya Iron,Manganese na Nitrogeni hivyo kufanya  mmea kuwa wa njano.



UPATIKANAJI: Hupatkana kwenye mbolea ya DAP ,NPK


Upungufu wa phosphorous kwenye Mahaindi.








3. POTASSIUM (K)

              Kirutubisho hiki husaidia mmea yafuatayo

·         Husaidia mmea kujitengenezea chakula chake  kwani ni muhusika mkuu kwenye kufunga na kufunguka kwa matundu ya stomata

           umbo ,ukubwa ,radha na rangi ya tunda ni kazi ya potassium

·         Hiki ni kirutubisho kinachohitajika sana na mmea baada ya Nitriogen



UPUNGUFU: Hufanya mmea kuwa njano pembezoni mwa jani huku  katkati jani likibaki kijani, pia hufanya majani kujikunja,na kuanguka kwa majani machanga na matunda.

KUZIDI:  Huathiri ukuaji wa mmea  kwani hufanya nitrogen isipatikane kwenye mmea hivyo mmea kuwa wa njano.

UPATIKANAJI: Hupatikana katika mbolea ya NPK.



UMUHIMU WA KIRUTUBISHO CHA POTASIUM (K)

·         Potasium ni kirutubisho muhimu sana baada ya nitorgen

·         Husaidia tunda kuwa na rangi nzuri na yenye kung’aa

·         Huongeza ubora wa punje

·         Husaidia kuongeza ukubwa wa tunda

·         Husaidia tunda kuwa na muonekano mzuri

·         Husaidia mazao kukaa muda mrefu baada ya kuvuna.






Umuhimu wa K kwenye Mahindi husaidia mmea  kupambana na ukame





v  VIRUTUBISHO SEKONDARI


                       1. CALCIUM

·         Calcium ni muhimu kwa afya ya mizizi, husaidia kutengeneza mizizi mipya

·         Huimarisha gamba la juu la tunda

UPUNGUFU: weusi kwenye sehemu ya chini ya tunda, kujikunja kwa majani machanga

KUZIDI: Huathiri upatikanaji wa Mgnessium na Potassium kwenye mmea

UPATKANAJI: CAN, Calcium Nitrate.


2.MAGNESIUM

·         husaidia utengenezaji wa chakula cha mimea

           UPUNGUFU: Unjano wa  majani pembezoni

           KUZIDI: Huathiri upatikanaji wa Calcium

3. SULFUR

·         Inasaidia kutengeneza protein kwenye mmea

           ni muhimu kwa mazao kama kitunguumaji na kitunguu swaumu 

           kwaajili ya harufu na kukuza mmea

UPUNGUFU: Hufanya mmea wote kuwa wa njano

KUZIDI: Mmea huwa wa njano

UPATIKANAJI: SA





UPUNGUFU WA MAGNESIUM 











VIRUTUBISHO VIDOVIDOGO
Virutubisho vidovidogo ni muhimu sana kwa ukuaji wa mimea kwani vikikosekana huathiri ukuaji wa mimea

Mfano:

BORON(B), CHLORINE(CL), COPPER(CU), IRON(Fe), MANGANESE(Mn) ,MOLYBDENUM(Mo),ZINC(Zn)








































MAMBO YAFUATAYO UNAPASWA KUFANYA ILI KUPTA MVUNO MENGI.

    1 Uchaguzi wa mbegu bora 
    2.Uwekaji wa mbolea kwa mda unaofaa
    Kupandia DAP, Kukuzia Urea, Kubebeshaea CAN kwa kifuniko kimoja kinatosha cha maji   kwa kila mhindi

3. Utumiaji wa dawa za mgugu au kufanya palizi  mapema.
4.Panda kwa kutumia nafasi
5.Piga dawa za wadudu kwa mda unaofaa.   

Natumaini msomaji wetu umenufaika na taarifa hii kwa ushauri waweza kutupigia simu 
kwa namba zifuatazo 
+255 719 886 932













 







Friday, 2 June 2017

TEAK PRODUCTION

1.   
   UZARISHAJI BORA WA MITIKI
                       http://agricomlizy.blogspot.com
                                By Faraja Israel Lwoga
                                Field Agriculture Officer
                              Cell no. +255 719 886 932









agriculturecomlizy.blogspot.com
        UTANGULIZI
Mitiki ni mti unaotengemewa na watu wengi kutokana na ubora wake hasa katika uimara wa mbao zake kwani huteleza na hung’aa sana pia mchwa hawawezi kushambulia mti huu,  Jina kamili ni (Teak tree) tectonagrandis.
UANDAJI  WA MBEGU
Ø                             Mbegu ya mtiki inatakiwa kulowekwa kwenye maji kwa siku tatu na kila baada ya     masaa kumi na mbili unamwaga maji na kuweka mengine hii ni kwasababu ya     kuondoa sumu iliyo kwenye maganda yake ya nje kwa sababu ni magumu ambayo                   mche hauwezi kutoka kiurahisi, Au unaweza kusugua maganda kwa kutoa (hard                    cort) ngozi ngumu ya mbegu ya mtiki baada ya kufanya hivyo unawaga kwenye kitaru            kilicho tayarishwa vizuri kulingana na idadi ya miche unayohitaji kuotesha unaweka               (farm yard manure) mbolea ya ngombe au ya kuku, au udongo wenye lutuba ambao ni           mweusi (dark soil).
                Njinsi ya kuaandaa udogo wa kuchanganya ni udogo wa msituni,mbole za            wanyama kama kuku,ng’ombe,mbuzi n.k ,pumba za mpunga na mchanda  (forest soil,manure,rice polish&sand) kwa uwiano wa  3:2:1:1  hii itasadia mmea kupata hewa ya kutosha kwenye viriba na kuhifadhi unyevu vizuri kwenye viriba yako mkulima,
  •       Unamwagilia maji kabla ya kusia mche au mbegu, unaweza kupanda moja kwa moja mbegu au kupanda miche kutoka kwenye kitaru chako kilicho tayarishwa vizuri.
agriculturecomlizy.blogspot.com
 UPANDAJI WA MTIKI
         Upandaji wa mitiki huafanyika mara baada ya mvua za kwanza kuanza kwa sababu                  ukuaji wa miche midogo huitaji mvua za kuendelea kwa kipindi kirefu, pia mvua za                  kwanza huwa na nitrogen ya kutosha kusaidia ukuaji wa mimea.
  • Vipimo vya upandaji kati ya mche na mche ni mita 2.5 mpaka 3, kama utatumia kipimo cha mita 3 kwa 3 ekari moja (mita 70 kwa 70) itaingia miche 530 kwa wastani. Miche ya mitiki hubananishwa wakati wa upandaji ili kuisaidia ikue kwa kunyooka kwenda juu ingawa mingine ya katikati itapunguzwa baada ya miaka 5-6 kuipa nafasi ile iliyobaki kama 260 iweze kunenepa     zaidi.
  • Mashimo ya mitiki hayahitaji kuchimbwa kabla kwa sababu yanaweza kufukiwa na mvua, kwa kawaida mashimo haya yana kuwa na urefu usiozidi futi moja (urefu wa rula ya mwanafunzi yaani cm 30) kwa hiyo siku ya upandaji wachimbaji wa mashimo ndio wawe wapimaji wa nafasi kati ya mti na mti. Wale wapandaji wahakikishe kwamba sehemu ya mzizi inakuwa chini ya ardhi na imefunikwa na udongo yote na sehemu ya shina inakuwa juu.
  • Miti kishapandwa iachiwe sehemu kidogo ya kisahani kwa ajili ya kuhifadhia maji kidogo, nyasi kidogo zinaweza kuwekwa kuzunguka shina ili kuzuia unyevu kunyonywa na jua (evaporation) ingawa hii wakati mwingine inaweza kuwavutia mchwa wakashambulia miche  yako.
  • Miche ikianza kuchipua baada ya siku chache vichipukizi zaidi ya kimoja vitachipua, hapa inatakiwa uvikate vyote na kubakiza chenya afya (viwili vitakuwa sawa)


Upandaji wa mitiki hufanyika katika namna mbili, wa kwanza ni ule wa kupanda miche ikiwa mizima kutoka katika vifuko na ya pili ni kutumia miche toka kwenye kitalu ambako inashauriwa kuing'oa na kisha kukata sehemu ya mzizi na shina, ambako utabakiwa na mzizi 70% na shina 30%.

Kitaalamu miche iliyokatwa na kubaki kama vipandikizi ina sifa mbili kubwa
agriculturecomlizy.blogspot.com
Miche ikiwa kwenye vifuko safi kwaajili ya kukua


(a) Miche itakayoota katika vipandikizi hivi ina uwezo mkubwa wa kuhimili ukame iwapo kutakuwa na upungufu wa mvua za msimu wakati wa upandaji. Mara nyingi miche ikipandwa kwenye mvua pungufu hufa sehemu ya juu ya shina/mche na sehemu ya chini ya mzizi kama vile miti inavyopukutisha majani, na hii husaidia kuhifadhi maji ndani ya mmea. Sasa kabla hili halijatokea sisi tunakata kabisa hizo sehemu zitakazo kufa iwapo kutakuwa na mvua pungufu.

(b) Miti inayoota katika vipandikizi inaasilimia kubwa zaidi ya kukua kwa kunyooka kwenda juu, wakati miti iliyokulia kwenye vifuko ina uwezo zaidi ya kupinda kwa sababu wakati wa uotaji ikiwa midogo, miche hushindana kukua na kukimbilia mwanga wa jua. Wakati huu ndio mche huanza kupinda kufuata mwanga ili kushindana na ile iliyokua haraka. Ili kuepuka hili, kata miche yako na ianze kuchipua upya ikiwa shambani kwenye nafasi.

Vipandikizi vilivyokatwa vinauwezo wa kukaa mpaka siku 7 bila kufa hadi siku ya kupandwa shambani, kwa maana hiyo unaweza kuvisafirisha toka mkoa mmoja hadi mkoa mwingine kwenda kuvipanda. Kama utakuwa umeandaa vipandikizi vyako na mvua zikawa bado kuanza, weka udongo kwenye chombo chochote mwagia maji kidogo (yasituame) halafu chomeka vipandikizi vyako na usubiri siku ya mvua kuanza ili ukavipande


Kabla ya kupanda miche ya mitiki shamba ni lazima liwe limeandaliwa, uandaaji wa shamba ni lazima ufanyike mapema kabla ya mvua kuanza kunyesha kwa sababu upandaju huanza mara baada ya mvua za kwanza kunyesha.
Uandaaji wa shmba la mitiki ni wakawaida kama ule wa mashamba mengine, visiki vyote ni lazima ving'olewe kisha majani yote yalimwe na ikiwezekana yatiwe moto kwa umakini wa hali ya juu kuepusha madhara ya moto.

Kama ulimaji utakuwa ni wa trekta au kutumia jembe la kukokotwa na wanyama (plau) hii ni nzuri zadi kwa sababu majani yatafukiwa ardhini na kuongeza rutuba kwenye udongo. Uuaji wa magugu kwa kutumia madawa kama Round up wanamazingira huwa hatushauri, ingwa ni njia moja ya haraka na nafuu zaidi kuliko kulima kwa jembe lolote lile.

Kwa ukanda wa pwani mvua za masika huanza kati ya mwezi wa 3 - 4 kwa hiyo ni vizuri sana kama utaanza kuandaa shamba kwenye mwezi wa 2 (February) na mvua za vuli huanza kwenye mwezi wa 11 (November) kwa hiyo shamba liwe tayari kwenye mwezi wa 10 (October)....
agriculturecomlizy.blogspot.com
Mkurugenzi


Kwa msaada zaidi 
Wasiliana nami kupitia
+255719 886 932
Email: flwoga_9196@outlook.com
flwoga629@gmail.com 



UKITAKA MICHE YA MITIKI
Wasiliana na Mkurugenzi
Kilimo Bora,
0753 797722/0719886932
(01:30 asubuhi hadi 09:30 alasiri)

agriculturecomlizy.blogspot.com

Friday, 26 May 2017

UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI


Ufugaji huu ni wa kienyeji kabisa ila huu umeboreshwa kidogo ili kuleta faida zaidi, kwanza itabidi uwe na eneo lakutosha,banda la kuku liwe linalohamishika au liwe limejengwa juu juu, hii husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa kwa sababu kinyesi cha kuku kikilundikana huweza kubeba vimelea vya magonjwa au liwe banda kubwa ambalo lina ngazi au mapumba chini ya sakafu ya banda kuepuha magonjwa.

AINA YA UFUGAJI WA KUKU.
1.Kufugia Huria.
Kuku huachwa wenyewe kujitafutia chakula na maji.Njia hii inatumika zaidi kufugia kuku wa kienyeji.Mara chache sana mfugaji huwapatia chakula cha ziada.
Ufugaji huu lazima uwe na eneo la kutosha kuku kuzunguka na kutafuta chakula.
Faida zake
Ø Ni njia rahisi ya kufuga.
Ø Gharama yake pia ndogo
Ø Kuku wanapata mazoezi ya kutosha.
Ø Kuku wanapata chakula mchanganyiko abacho kinafaa kiafya.
Hasara zake
Ø Kuku wanakuwa hatarini kuibiwa au kudhurika na wanyama wakali na hali mbaya ya hewa.
Ø Ukuaji wa kuku ni hafifu hufika uzito kilo 1.2 baada ya mwaka.
Ø Nirahisi kuambukizwa magonjwa.
2.Kufuga nusu ndani-nusu nje (Semi-intensive)
Huu ni ufugaji ambao kuku wanakuwa na bandalililounganishwa na uzio kwa upande wa mbele.
Hapa kuku wanaweza kushinda ndani ya banda au nje ya banda wakiwa ndani ya uzio.
Faida zake
Ø Kuku wanakuwa salama mbali na madui mbalimbali
Ø Utaweza kuwalisha kuku vizuri hivyo wataweza kuongeza uzalishaji wa mayai na nyama ( kwa kukua haraka )
Ø Itakuwa rahisi kwako kudhibiti wadudu na vimelea vinavyoweza kuleta magonjwa kwa kuku.
Ø Ni rahisi kuwatenganisha kuku kwa makundi tofautitofauti na kuwaudumia ipasavyo.
Ø Rahisi kuwatambua kuku wagonjwa kuliko kufugia huria.
Changamoto za kufugia nusu ndani nusu nje.
Ø Hauna budi uwe na mda wa kutosha kwa ajili ya kuwahudumia kuku wako.
Ø Pia utaitaji kuwa na eneo kubwa kiasi cha kutosha kufugia
Ø Pia utahitaji kuingia Gharama ya ziada kidogo ya kutengeneza wigo na banda na kuwapatia kuku chakula cha ziada .
Ø Utahitaji kuwa na vifaa vya kulia chakula na maji

3. Kufugia ndani ya Banda tu.
Njia hii kuku huwa ndani ya banda tu, Katika njia hii kuku hukaa ndani ya banda mda wote,
Njia hii ya ufugaji utumiwa na wafugaji wa kuku wa kiasasa kama (Broiler for meat purpose and Layer for egg production)  
Lakini unaweza kutumika hata kuku wa asili hasa sehemu zenye ufinyu wa maeneo.
Faida zake
Ø Nirahisi kutambua na kudhibiti magonjwa.
Ø Ni rahisi kudhibiti upotevu wa kuku,mayai na vifaranga
Ø Ni rahisi kuwapatia chakula kulinga na mahitaji ya kila kundi.
Ø Ni rahisi kuwatambua na kuwaondoa kuku wasiozalisha Katika makundi.
Changamoto za Ufugaji wa Ndani ya Banda tu.
Ø Unatakiwa uwe na mda wa kutosha wa kuwahudumia kuku wako kikamilifu.
Ø Pia unatakiwa kuwa na mtaji mkubwa wa kujenga banda na kuwanunulia kuku chakula.
Ø Ugonjwa ukiingia ni rahisi kuambukizana. Vilevile kuku huweza kuanza tabia ya kudonoana.
NB; Ni muhimu kuhakikisha kuku wako wanapata chakula cha kutosha chenye virutubisho vyote vinavyohitajika unapoamua kutumia mfumo wa ufugaji wa kuku wa ndani.
 
BANDA BORA
Banda liwekewe viota vya kutagia na unaweza kuwafundisha kuku kuvitumia mapema kabla ya kuanza kutaga kwa kuchelewa kuwafungulia asubuhi. Kwa kawaida kuku hupenda kulala bandani wakiwa juu juu kwa hiyo uweke baadhi ya fito au mbao nyembamba zikining’inia pia kuwe na vyombo vya chakula nje ya banda
Hakikisha banda halivuji na wanyama wakali hawaingii lakini liwe na hewa ya kutosha na lisiwe na joto wala baridi kali, ni vizuri ukiliweka chini ya miti
Ili kuboresha ufugaji huu inashauriwa kutumia majogoo ya kisasa ambayo yana patika kwa mazalishaji wa kuku kote nchini, pia unaweza kutumia majogoo ya kuku aina ya
KUCHI wanaopatikana zaidi miko ya Singida na Shinyanga. Majogoo ya kisasa huweza kuhudumia wastani wa majike 20-25 na KUCHI huweza kuhudumia majike 10 -15 kwa sababu ni wavivu kidogo
Andaa na banda la kukuzia watoto ambalo litawakinga na wanyama wakali na mwewe, banda linakuwa wazi juu hukulikizuiwa na waya kwa 75% na 25% iwe imezibwa kwa mbao ili kuwapatia kivuli wanapohitaji, banda hili lina hitaji kuhamishwa hamisha angalau mara 5 kwa siku kutika mahali pamoja hadi pengine, hakikisha banda la watoto lina maji na chakula muda wote, pia kumbuka kuwawekea mabaki ya mboga za majani kama mchicha, kunde, kisamvu n.k

Banda hili pia waweza tumia kwa kukuzia vifaranga au kutagia mayai.


Banda hili linaanza kujenjwa kwa matofali kwenye msingi.
Mahitaji ya kujenga banda hii
Ø Mabati
Ø Misumali
Ø Mbao
Ø Tofari
Ø Sumenti
Ø Wirenet au waya wa Senyenje na hii itasababisha kuku kupata hewa ya kutosha

MABANDA YA KISASA
Banda hii linauzo wa kufuga kukuhadi 3000
























Upana 10 m*Urefu 80m
Mahitaji yakujenga Banda hii
Ø Eneo 1300m kwa (semi-intensive)
Ø Mabati
Ø Mbao
Ø Senyenge wire
Ø Tofali kwaajili ya msingi
Ø Sumenti
Ø Misumali
Banda lenye uwezo wa kuku 600

Upana 5m*urefu 20m
Mahitaji ya Banda hii
Ø Eneo 150m
Ø Mabati
Ø Wire
Ø Mbao
Ø Matofali
Ø Sumenti
Ø Misumali
  • CHANJO ZA KUKU
Kuku wapewe chanjo ya kideri/mdondo kila baada ya miezi mitatu chanjo hii hupatikana nchini kote ukifika dukani ulizia chanjo ya newcastle, utapata maelekezo ya jinsi ya kuwawekea kuku kwenye maji ya kunywa, chanjo hii wapewe kuku wazima tu na wagonjwa watengwe mbali
  • MINYOO YA KUKU 
Kuku hunyweshwa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, kuna dawa kama piperazine na nyinginezo ambazo huwekwa kwenye maji
  • CHAWA NA UTITIRI
Unaweza kutumia dawa za kuogeshea mifugo kama ecotix au dawa ya unga unga ya kunyunyuzia kama akheri powder, dawa ya akheri unaweza kuimwaga bandani na kisha kumnyunyuzia kuku mwilini ukiwa umemning’iniza kichwa chini miguu juu ili mayoya yaacha nafasi ya dawa kuingia
  • MAGONJWA YA MAPAFU
Kuna magonjwa mengi yanayoshambulia mfumo wa hewa, dawa ya tylosin inauwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa karibu yote, wape dawa hii mara tu unapoanza kuona dalili za mafua
MAGONJWA YA KUKU,DALILI, NA TIBA ZAKE
Kila ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha na magomjwa mengine, ingawa zipo zile za kufanana mfano kutokula vizuri, kushusha mabawa, kuzubaa/kusinzia na joto kuwa juu
 NEWCASTLE /KIDERI / MDONDO
Dalili kuu: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba. kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30% na mult vitamini.
GUMBORO / INFECTIOUS BURSAL DISEASE.
Dalili kuu:Kuharisha rangi nyeupe kama chokaa. Ukimpasua baada ya kufa kunakuwa na kama matone ya damu kifuani na kwenye firigisi sehemu ya mbele
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.
MAREK'S DESEASE/ MAHEPE
Dalili kuu:kuparalyse /kukakamaa and kwa miguu na mabawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kihifadhia chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5 wakianza kutaga.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.
NDUI YA KUKU / FOWL POX.
Dalili kuu:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya kama vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba., kupunguza madhara waoshe kwa maji ya uvugu vugu yenye chumvi ya mawe hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic kama Otc 20%.
 MAFUA MAKALI/ INFECTIOUS CORYZA
Dalili kuu:Chafya, kusinzia, kuvimba sehemu za  uso, kichwa  na macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, udenda puani na mdomoni.
Tiba: Fluban, au  Tylodox au OTC 20 %, Tylosan, changanya na mult vitamini.
 FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO
Dalili Kuu:Mharo rangi ya njano.
Tiba: Esb3, Trimazine 30%, Tylodox.

COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU.
Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu.
Tiba: Amprolium 20%,Esb3, Trimazine 30%, Vitacox, na Agracox.
FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU.
Dalili kuu: kinyesi mharo wa kijani.
Tiba: Trimazine 30 % au Esb3.
MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKANAYO NA LISHE DUNI
Dalili kuu:Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.
Tiba: Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa mult vitamin na protein, kwa wanaodonoana kata au choma midomo yao na uwape mboga za majani ukiwa umezining'iniza juu kidogo.

VYAKULA
Vifaranga
Vifaranga
Kuku
Anza
Kuzia
Mayai taga
Kiasi(kg)
kg
kg
kg
Mahindi sagwa
38
28
20
Pumba mahindi
19
24
30
Pumba mpunga
19
24
30
Mashudu alzeti
08
08
06
Mashudi Pamba
00
02
06
Dagaa sagwa
10
07
03
Damu sagwa
04
05
02
Chokaa Mifugo
01
01
02
Madini Mchanganyiko
0.5
0.5
0.5
Chumvi sagwa
0.5
0.5
0.5
Jumla
100kg
100kg
100 kg
NB:
Kama utawapa kuku wako wa wanaotaga mayai dawa zenye sulphur ndani watapunguza kutaga mayai, kwa hiyo kama utaweza kupata dawa ambayo haina sulphur ndani yake itakuwa ni vizuri zaidi.


agriculturecomlizy.blogspot.com
agriculturecomlizy.blogspot.com
Prepared, 
KILIMO BORA,
Agriculture Field Officer
Faraja Israel Lwoga.
phone: +2557198886932.





AGRICOMLIZY®

KILIMO CHA MAHINDI

MAHINDI Mahindi ni zao muhimu sana katika kilimo hapa nchini na hukuzwa na takribani 70 % ya wakulima wa hapa Tanzania. Maeneo yanayoongo...